Jumatatu 6 Oktoba 2025 - 16:01
Kujitolea kwa Harakati ya Muqāwama ya Palestina Hatimaye Kutausambaratisha Utawala wa Israel

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Nāzir Abbas Taqvī, katika hotuba yake, huku akisisitiza uimara wa Muqāwama wa Palestina alisema: “Kujitolea kwa wananchi na wapiganaji wa Palestina hatimaye kutausambaratisha utawala wa kigaidi wa Kizayuni, na ushindi wa mwisho utakuwa ni wa taifa la Palestina.”

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Wanafunzi Imamiyya Pakistan katika mji wa Karachi iliandaa maandamano ya upinzani yakiwa na kauli mbiu isemayo: “Israel haikubaliki”. Washiriki wa maandamano hayo, pamoja na kulaani vikali sera na makubaliano ya Marekani, walisistiza kushikamana daima na malengo na fikra za mwanzilishi wa Pakistan, Qa’id-e-Aʿẓam Muhammad Ali Jinnah, wakaonesha mshikamano wao na taifa la wanyonge la Palestina na kutoa heshima kwa juhudi na kujitolea kwa viongozi wa Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌.

Hujjatul-Islam Nāzir Abbas Taqvī, Katibu Mkuu na mwanachama mwandamizi wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika hotuba yake alisema:

“Tarehe 7 Oktoba inatimia miaka miwili ya Muqāwama, na leo mafanikio ya Muqāwama yamebainika kwa kila mmoja. Mashahidi na waliojitoa mhanga katika njia ya Muqāwama ndio watakao sababisha anguko la karibu la Israel, kwani sheria ya Mwenyezi Mungu inasisitiza kuangamizwa kwa dhulma.”

Aliongeza kwamba watawala wa Kiislamu wamekwama katika siasa za maelewano, na kupokea makubaliano ya amani ya Marekani kutawadhalilisha Waislamu milioni 250.

Hujjatul-Islam Muhammad Sadiq Jafari, mjumbe mwandamizi wa Majlis Wahdat-e-Muslimeen Pakistan, katika hotuba yake alisema wazi:

“Tunayakataa kwa ukamilifu makubaliano ya amani ya Marekani na daima tutaendelea kushikamana na fikra za Kiongozi wetu.”

Wajumbe wa Baraza la Maimamu wa Misikiti na Wanazuoni wa Imamiyya Pakistan pia, katika hafla hii, walizungumza kuhusu historia ya Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌, wakibainisha kuwa licha ya kusimamishwa takriban asilimia 90 ya meli, bado meli nne ziliweza kuendelea na safari yao — jambo linalodhihirisha nguvu na azma ya Muqāwama.
Walisema kwamba hatua za Sayyid Ḥasan Naṣrullāh na mashahidi wa Muqāwama zilituma ujumbe wa wazi duniani kwamba vitisho vya Netanyahu vimehukumiwa kushindwa.

Hujjatul-Islam Mubashir Hasan, akirejelea hali mbaya ya Gaza, alisema:

“Watu wa Gaza wanateseka kutokana na njaa na magonjwa. Seneta Mushtaq Ahmad ni shujaa wa kitaifa. Serikali inapaswa mara moja kuwasiliana na jamii ya kimataifa ili kufanikisha kuachiliwa kwake.”

Wasemaji waliendelea kusema kwamba: “Kwa bahati mbaya, muuaji mkubwa wa dunia Trump amependekezwa kuoewa Tuzo ya Nobel.”

Yāwar Abbas naye aliifananisha Palestina ya leo na Karbala ya zama hizi, akamtaja Sayyid Ḥasan Naṣrullāh kuwa ni “Alamdar” (mshika bendera) wa Karbala ya kisasa, na akasisitiza kuwa baadhi ya nchi za Kiislamu katika zama hizi zinacheza nafasi sawa na Watu wa Kufa katika tukio la Karbala.

“Tunawasalimu hawa watangulizi wa haki za binadamu — wale ambao kwa kuhatarisha maisha yao, wamesimama kuwatetea watu wanyonge wa Palestina. Ujasiri wa Seneta Mushtaq Ahmad, ambaye kwa sasa yuko gerezani mikononi mwa majeshi ya Israel, unastahili pongezi kubwa.”

Maandamano haya ni ishara ya mshikamano wa kina wa taifa la Pakistan na watu wa Palestina, na pia ni onesho la uungaji mkono imara wa haki za binadamu na uadilifu katika eneo hili, huku akisisitiza kuunga mkono Muqāwama wa Palestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha